Question

1. Chagua kivumishi cha sifa kinacholingana na nomino ya wingi ya ngeli ya N-N.

A. Nyumba nzuri zimejengwa.

B. Mbwa wazuri wamecheza.

C. Viatu vizuri vimevalika.

D. Magari makubwa yamepaki.


2. Ni kivumishi kipi kiashiria kinachofaa kukamilisha sentensi: "Mji ______ umepata maendeleo makubwa." (hiyo / huu)

A. Huu

B. Hiyo

C. Ile

D. Yule


3. Chagua sentensi iliyo na kivumishi cha idadi kinacholingana na nomino yake.

A. Wanawake tatu wamesimama.

B. Kalamu mbili zimepotea.

C. Mti miwili imepandwa.

D. Viti nne vimevunjika.


4. Ni kivumishi kipi kiulizi kinachouliza kuhusu mahali?

A. Lini

B. Wapi

C. Nini

D. Jinsi gani


5. Unganisha sentensi: "Mvulana ameanguka. Mvulana alikuwa akicheza." kwa kutumia kivumishi kirejeshi 'amba-'.

A. Mvulana ambaye alikuwa akicheza ameanguka.

B. Mvulana ambacho alikuwa akicheza ameanguka.

C. Mvulana ambao alikuwa akicheza ameanguka.

D. Mvulana ambapo alikuwa akicheza ameanguka.


6. Chagua sentensi iliyo na kivumishi cha nafsi kilichotumika vibaya.

A. Ndege yangu imeruka.

B. Kitabu lako kimepotea.

C. Watoto wenu wamelala.

D. Macho yao yanaona.


7. Ni ipi kati ya hizi ni kiwakilishi cha idadi?

A. Wanafunzi wengi

B. Wote wamefika

C. Mbwa watatu

D. Maji chache


8. Katika sentensi "Mama alipika chakula tamu lakini hakuwa na muda wa kutosha," neno 'lakini' linafaa kuongozwa na alama gani ya uakifishaji?

A. Nukta (.)

B. Mkato (,)

C. Alama ya kuuliza (?)

D. Alama ya mshangao (!)

Powered by Froala Editor

Answer

1. A. Nyumba nzuri zimejengwa.

"Nyumba" ni nomino ya ngeli ya N-N

Ngeli ya N-N ni ya kipekee kwa kuwa kivumishi cha sifa hakibadiliki kwa umoja au wingi.

Kivumishi kama "nzuri", "mbaya", "ndogo", "nene" nk. hubaki hivyo hivyo kwa nomino kama: nyumba, barua, meza, dawa, mbwa, ndege, etc.

B. ‘Mbwa’ iko katika ngeli ya A-WA

C. ‘Kiatu’ iko katika ngeli ya KI-VI

D. ‘Gari’ iko katika ngeli ya LI-YA


2. A. Huu


3. B. Kalamu mbili zimepotea.

‘Kalamu’ iko katika ngeli ya I-ZI

A. ‘Mwanamke’ iko katika ngeli ya A-WA, sentensi yafaa kuwa; Wanawake watatu wamesimama.

C. ‘Mti’ iko katika ngeli ya U-I, sentensi yafaa kuwa; Miti miwili imepandwa.

D. ‘Kiti’ iko katika ngeli ya KI-VI, sentensi yafaa kuwa; Viti vinne vimevunjika.


4. B. Wapi

‘Wapi’ huuliza kuhusu mahali

A. 'Lini' huuliza kuhusu wakati.

C. 'Nini' huuliza kuhusu kitu.

D. 'Jinsi gani' huuliza kuhusu namna.


5. A. Mvulana ambaye alikuwa akicheza ameanguka.


6. B. Kitabu lako kimepotea.

'Kitabu' ni ngeli ya Ki-Vi, kivumishi cha nafsi kinapaswa kuwa 'chako', si 'lako'


7. B. Wote wamefika

"Wote" ni kiwakilishi cha idadi kwa sababu inachukua nafasi ya nomino, na huonyesha jumla ya watu


8. B. Mkato (,)

Mkato hutumika kabla ya viunganishi kama 'lakini' vinavyounganisha vifungu huru.

Powered by Froala Editor

Back to Questions